Ideas for Play.
Tambua kitu kwa kivuli chake
Shika kitu cha nyumbani mbele ya mwanga wa tochi. Kisia ni kitu gani kimetoa kivuli ukutani.
Unachohitaji
- Tochi au taa
- Ukuta wa rangi nyepesi
- Vitu vikubwa vitatu au vinne vya nyumbani
Jinsi ya kucheza
Punguza mwanga chumbani na uangaze tochi au taa kwenye ukuta wa rangi nyepesi.
Mwombe mtoto afumbe macho huku ukishika kitu mbele ya mwanga.
Aangalie kivuli akisie ni kitu gani.
Mwonyeshe kitu hicho mkilinganishe na kivuli chake.
Badilishaneni nafasi ili mtoto achague kitu na wewe ukisie.
Jaribu kukigeuza kwa upande ili iwe vigumu zaidi kukitambua.
Mawazo ya kujaribu
- Uma au kifaa cha kupigia mayai
- Kikombe chenye mpini
- Dubu wa kuchezea
- Ndizi
Kwa nini ujaribu?
Mtoto anatambua kitu halisi kutokana na umbo bapa kisha anapata zamu ya kutega kitendawili.
Mambo ya kuangalia
Je, anatambua kuwa kitu kilekile hutoa vivuli tofauti kikigeuzwa?
Rekebisha mchezo umfae mtoto wako
- Njia nyingine za kushiriki
- Chagua vitu anavyovifahamu na anavyoweza kugusa kabla ya mchezo.
- Rahisisha mchezo
- Onyesha vitu vyote kwanza, kisha akisie ni kipi.
Usalama
Kaa karibu.
- Msitazame moja kwa moja kwenye taa au mwali wa tochi.
- Wekeni taa na nyaya zake mahali thabiti pasipozuia njia.